ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dkt.Hussein Ali Mwinyi amejumuika na wananchi katika mazishi ya marehemu ya Mahad Ali Suleiman aliyefariki jana wakati akitibiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt.Mwinyi amewaongoza Waumini wa Dini ya Kiislamu katika sala ya maiti Msikiti Jammiu Zenjibar Mazizini Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi.
Marehemu amezikwa kijijini kwao Fujoni Wilaya ya Kaskazini B, Mkoa wa Kaskazini Unguja tarehe 24 Aprili 2025.