Rais Dkt.Samia aipongeza Simba SC kwa ushindi dhidi ya Stellenbosch FC

ZANZIBAR-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan ameipongeza Simba SC kwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Stellenbosch FC ya Afrika Kusini.
Ni katika mchezo kwa kwanza wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho barani Afrika uliofanyika Aprili 20,2025 katika Dimba la New Amaan Complex.

“Hongera sana kwa Klabu ya Simba kwa ushindi katika mchezo wa Mashindano ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika (CAF Confederation Cup).

“Mmeleta furaha kwa mashabiki wenu na Watanzania wote na kuipeperusha vyema bendera ya nchi yetu.

"Motisha kutoka kwangu mtaipokea kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Ninawatakia kila la kheri,” ameandika Rais Dkt.Samia kwenye ukurasa wake rasmi wa mitandao ya kijamii.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news