DAR-Serikali imeufunga Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam kwa muda kuanzia Aprili 9, 2025 ili kupisha marekebisho ya eneo la kuchezea (pitch) lililopata athari kubwa kufuatia mvua zilizonyesha zilizofuatiwa pia na mechi ya robo fainali Kombe la Shirikisho Afrika kati ya Simba SC na Al Masry ya Misri.
Taarifa rasmi ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imeeleza kuwa,Timu ya Wataalamu itaanza mara moja kufanya tathmini ya kina ya madhara yaliyojitokeza na tarehe ya kufunguliwa kwa uwanja huo itatangazwa hapo baadae.