RIYADH-Tanzania na Saudi Arabia zimesaini Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano Katika kuendeleza Sayansi na Elimu.
Hati hiyo ya Ushirikiano imesainiwa tarehe 13, Aprili, 2025, jijini Riyadh nchini Saudi Arabia kati ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ya Tanzania na Wizara ya Elimu ya Saudi Arabia ikilenga kuendeleza Sayansi Teknolojia na Elimu.
Hati hiyo ya Makubaliano imesainiwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda na Waziri wa Elimu na Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji ya HCDP ya Saudi Arabia Mhe. Yousef bin Abdullah Al-Benyan.

Tukio hilo limeshuhudiwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Lela Muhamed Mussa, Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Dkt. Moh’d Juma Abdalla, Katibu Mkuu Wizara ya elimu Sayansi na Teknolojia Prof.Carolyne Nombo, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Wakurugenzi na maafisa wengine wa Wizara ya elimu