NA MWALIMU TUMAINI MASHINGO
TUNDU Lissu anapaswa kurudi tena darasani kusoma nini maana ya siasa kabla ya kile chama cha Ufipa kumfia, anapaswa kukutana na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kama atatia nia, maana ile siasa yake na siasa ya Chama chao ni CCM level ya Tawi la Chuo Kikuu ambayo inaishi kwa visasi au heshima ya kambale mkubwa ndevu na mtoto ndevu, anapaswa kufika shuleni Kizimkazi.
Kwa ilivyo ninamuona ana kipaji cha kuchekesha apatiwe namba ya Coy Mzungu akiwa serious yeye na Eliud watatisha, anaitaka nchi wakati ameshindwa kutibu majeraha ya wachache, anaitaka nchi wakati ameshindwa kuunganisha roho zilizokinzana, anaitaka nchi wakati watu kadhaa tu ameshindwa kuwaongoza, apatiwe namba za Coy Mzungu haraka kama anaiwaza Jamhuri iwe mkononi mwake.
Yule Antipass anapaswa tena kufanyiwa udahili wa kisiasa, kwa kuwa ana ufaulu mzuri kidato cha sita basi asogee shuleni Kizimkazi kukumbushwa chama cha siasa hakiendeshwi kama kikoba, hakitumi meseji WhatsApp kumtengua mwanachama, tupo kuwakumbusha misingi ya Utu, Nidhamu na kufuata Katiba yao.
Mwambieni Antipass anaweka matundu kwenye mioyo ya wana Ufipa, kama vifungu vichache vya Katiba ya chama chao havifahamu ataweza Katiba ya Jamhuri? Kama watu wachache wanampelekesha ataweza kubeba maono ya Watanzania? Inafikirisha na kuwazisha, inachekesha pale ni Chamani ama Watu Baki, tumpatie namba za Coy wa Cheka Tu?.
Inachekesha anayehubiri demokrasia anaiendesha Ufipa kwa mkono wa chuma, nasikia vikaoni huruhusiwi kuhoji, maelekezo yakitoka Nairobi yanapaswa kupokelewa kama yalivyo hupaswi kuedit script, waliokuwa kambi nae tofauti wakati wa uchaguzi wanaishi kama wakiwa, wanakiona cha moto na mmoja mmoja anashughulikiwa, inatisha na kuogopesha kwa yule aliyejiita mwanademokrasia na sasa amevua kofia tukiona sura yake halisi inafurahisha sana, Tundu anapaswa kurudi Kizimkazi University ale nondo za kuongoza chama.
Mwalimu nasema uamuzi ni wake, akitaka siasa safi ya kufika mbali na Ufipa majibu yako Kizimkazi, aje tumpe form ajiunge ale darasa, Demokrasia anayoitaka ipo CCM, ukweli na uwazi anaotaka Upo CCM, aje Kizimkazi tumpe form ila kama anasikiliza kutoka Nairobi basi Coy Mzungu tutampatia namba zake aende akachekeshe maana kwa yanayoendelea sasa ni zaidi ya Cheka Tu na Watu Baki.
Tags
Habari
