Tuzindue mpango wa ujuzi kwa vijana katika uchumi wa buluu-Rais Dkt.Mwinyi

LONDON-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema, ni muhimu kuzinduliwe mpango wa ujuzi wa vijana wa Jumuiya ya Madola ambao utawapa vijana milioni moja ujuzi katika sekta ya uchumi wa buluu na kijani ifikapo 2030.
Rais Dkt. Mwinyi amesema hayo leo Aprili 7,2025 alipozungumza katika Mkutano wa Biashara na Uwekezaji wa Jumuiya ya Madola (Commonwealth Trade & Investment Summit 2025) kwenye ukumbi wa mji wa kihistoria Mansion House, London unapofanyika mkutano huo.
Amehimiza kuanzishwa kwa ufadhili wa kujitolea na utaalamu katika sekta hiyo ili kuharakisha maendeleo endelevu ya bahari katika nchi za Jumuiya ya Madola.

Aidha, Rais Dkt.Mwinyi ametoa wito kwa washiriki wa mkutano huo kuitembelea Zanzibar na kujionea fursa za uwekezaji katika sekta ya uchumi wa buluu, utalii wa mazingira , nishati mbadala ya bahari, ufugaji wa samaki endelevu na maendeleo ya bandari.

Kwa upande mwingine, Rais Dkt.Mwinyi amesema dhamira ya Serikali ni kuhakikisha ifikapo Mwaka 2050 Zanzibar itakuwa ya uchumi wa kati baada ya kuzinduliwa kwa Dira ya Maendeleo kupitia mkakati wa sera ya uchumi wa buluu ya Mwaka 2022.
Mkutano huo umehudhuriwa na Viongozi mbalimbali kutoka Nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news