MORONI-Uongozi wa Chuo cha Benki Kuu ya Tanzania, watembelea Visiwa vya Comoro ikiwa ni sehemu ya jitihada za kupanua wigo wa huduma za mafunzo za chuo hicho nchini Comoro.
Uongozi huo ukiongozwa na Mkuu wa Chuo hicho Dkt.Nicas Yobu ambaye ameambatana na Mhadhiri Mwandamizi Bi.Asumpta Muna umewasili nchini Comoro na kupokelewa na Balozi wa Tanzania nchini humo, Mhe. Saidi Yakubu.

Baada ya kuupokea ujumbe wa uongozi wa Chuo hicho, Mhe. Balozi Yakubu alitumia nafasi hiyo kuufahamisha fursa mbalimbali zilizoko nchini Comoro katika sekta za fedha na benki.
Uongozi wa Chuo cha Benki Kuu katika ziara yao nchini Comoro unatarajiwa kuonana na Gavana wa Benki Kuu ya Comoro na viongozi wa benki zilizoko Comoro pamoja na Uongozi wa Chuo Kikuu cha Comoro.