DAR-Aprili 14,2025 Serikali ya Mtaa wa Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam ililiandikia barua Shirika la Reli Tanzania (TRC), kuomba Shilingi milioni 8,915,000 kwa ajili ya matengenezo ya kipande cha barabara cha mtaa na mtaro wa kupitisha maji yanayodaiwa kutoka kwenye tobo la maji lililotengenezwa na mradi wa SGR, maji hayo ilielezwa kuwa yanaelekea kwenye majumba ya watu kwa kuwa mfereji umeziba.
Chini ni video yenye mahojiano na Moshi Selemani Mwaluko ambaye ni Mwenyekiti Serikali ya Mtaa Gongo la mboto,Majula Alisdius Mtalemwa ambaye ni Afisa Mtendaji Kata Gongo la mboto,Lucas Lutainulwa ambaye ni Diwani Kata ya Gongo la mboto na Mhandisi Tadei Komu ambaye ni Meneja Mradi Msaidizi SGR Dar es Salaam-Morogoro. Endelea;