ARUSHA-Wanadiplomasia mbalimbali wapo katika ziara ya kitalii Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro mkoani Arusha. Bonde la Ngorongoro ni bonde (Creator) kubwa zaidi lisilo na mivunjiko duniani likiwa na mandhari ya kipekee ya kuvutia na wanyama aina tofauti wakiwemo wanyama watano wakubwa duniani.