Mkurugenzi wa TANESCO afariki kwa ajali

MARA-Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Aprili 13, 2025. Ni katika ajali iliyotokea wilayani Bunda mkoani Mara.
Mhandisi Nyamo-Hanga ambaye amedumu katika nafasi hiyo kwa mwaka mmoja aliteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan mwishoni mwa mwaka 2023. Pia,Mhandisi Nyamo-Hanga aliwahi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Umeme Vijijini (REA).

Mkuu wa Mkoa wa Mara, Evans Mtambi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, ambapo amefafanua kuwa limetokea kati ya saa 6 hadi 7 usiku wa kuamkia leo.

Wakati huo huo,Meneja wa TANESCO Mkoa wa Mara, Nickson Babu amesema,mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali Teule ya Wilaya ya Bunda huku wakisubiri taarifa zaidi kuhusu taratibu nyingine.
Katika kipindi cha mwaka mmoja,Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga amefanya mambo mengi chanya ambayo yamewezesha upatikanaji wa nishati ya umeme kuwa tulivu.

Aidha, kupitia Serikali alijitolea kuharakisha matengenezo yanayoendelea ya mitambo ya umeme,kusimamia miradi huku akijitahidi kukabiliana na tatizo la umeme nchini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news