Waziri Bashe apiga marufuku mazao ya kilimo kutoka Malawi na Afrika Kusini kuingizwa nchini

DODOMA-Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe, ametangaza uamuzi mgumu dhidi ya nchi ya Malawi na Afrika Kusini kwa kuzuia mazao yoyote ya kilimo kuingia nchini kutoka na nchi hizo kukakataa kubadili msimamo wao wa kuruhusu mazao kutoka Tanzania kuingia kwenye nchi zao.
Waziri Bashe ametangaza uamuzi huo usiku wa Aprili 23, 2025, huku akisema msimamo ni kupiga marufuku matunda kama apples na mengine kutoka Afrika Kusini kuingia nchini, hadi watakapoondoa zuio kwa Tanzania.

“Kuanzia usiku huu Aprili 23, 2025, hautaruhusu zao lolote linalotoka Afrika Kusini linalohusiana na kilimo kuingia nchini kwetu,

“Malawi hadi sasa hawajafuta notisi waliyoitoa dhidi ya Tanzania, Natangaza rasmi ni marufuku kwa mazao yoyote ya kilimo kuingia ndani ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzia leo. Kwa nchi zote mbili hasa Malawi hatutaruhusu zao lolote kupita nchini kwetu,”amesema.

Aidha, amesema wakati Malawi inawakatalia wafanyabishara wa Tanzania kupita lakini wao (Malawi) kupitia Shirika la Moja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) wananunua mahindi kwa hoja ya njaa, kwahiyo mahindi yote waliyonunua kwa ajili ya kutatua tatizo la njaa kwao hayatoenda Malawi, hatutayapeleka na wala hatutaruhusu WFP kuyapeleka hadi watakapofungua soko.

Waziri Bashe amesema Mei 1, 2025 walikuwa wanaanza kuchukua mbolea kutoka Tanzania kwa ajili ya msimu wa kilimo, hatutaruihusu mbolea yoyote kwenda Malawi.
“Hatua hii haihatarishi usalama wan chi wala usalama wa chakula , hakuna mtanzania atakufa kwa kukosa zabibu ya Afrika Kusini, hakuna mtanzania atakufa kwa kukosa Apple kutoka Afrika Kusini, Tunachukua hatua hii kulinda biashara yetu,”amesema Bashe.

Aprili 17, mwaka huu, Waziri Bashe alitoa siku saba kwa nchi za Afrika Kusini na Malawi kuondoa zuio la mazao ya Tanzania, vinginevyo hatua kali zitachukuliwa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news