Waziri Dkt.Nchemba afanya mazungumzo na Mkurugenzi wa IMF anayesimamia Kanda ya Afrika

WASHINGTON-Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), amekutana na kufanya Mazungumzo na Mkurugenzi wa Shirika la Fedha la Kimataifa -IMF anayesimamia Kanda ya Afrika, Bw. Abebe Selassie, kando ya Mikutano ya Majira ya Kipupwe ya IMF na Benki ya Dunia, inayofanyika jijini Washington D.C, nchini Marekani, ambapo wamejadiliana masuala mbalimbali ya ushirikiano ikiwemo utekelezaji wa programu ya Extended Credit Facility-(ECF), inayohusisha upatikanaji wa mkopo nafuu kwa ajili ya kuimarisha uchumi wa nchi kupitia sekta za uzalishaji na huduma za jamii pamoja na ufadhili wa kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi kupitia dirisha la Resilient and Sustainable Fund (RSF) kutoka Shirika hilo.
Kikao hicho kimehudhuriwa na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Mhe. Stanslaus Nyongo (Mb), Magavana Mbadala wa IMF na Benki ya Dunia, ambao ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Emmanuel Tutuba, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango-Zanzibar, Dkt. Juma Malik Akil, Naibu Gavana Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dkt. Yamungu Kayandabila, na maafisa wengine waandamizi wa Serikali na IMF.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news