MHESHIMIWA Jenista Mhagama (Mb), Waziri wa Afya na Mjumbe Maalum wa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amewasilisha Ujumbe wa Mhe. Rais Samia kwa Mhe. Russell Mmiso Dlamini, Waziri Mkuu wa Ufalme wa Eswatini aliyepokea kwa niaba ya Mfalme Mswati III wa nchi hiyo.