Yanga SC yaichapa Fountain Gate FC mabao 4-0

MANYARA-Young Africans Sports Club (Yanga SC) imeendelea kuusogelea ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara huku Clement Mzize akizidi kung'ara zaidi.
Ni baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Fountain Gate FC katika dimba la Tanzanite Kwaraa lililopo mjini Babati mkoani Manyara.

Kupitia mtanange huo wa Aprili 21,2025 Yanga SC wana alama 13 mbele ya watani zao Simba SC ambao hata hivyo, wana michezo minne mkononi.

Clement Mzize katika mchezo huo alifunga magoli mawili dakika ya 38 na 70 mtawaliwa na kufikisha jumla ya magoli 13 kwenye msimamo wa ufungaji bora kwenye Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara.

Bao la tatu lilitumbukizwa nyavuni na Stephanie Aziz Ki dakika ya 43 mtawaliwa huku Clatus Chama akifunga bao la nne dakika ya 89 mtawaliwa.

Kwa matokeo hayo,Yanga SC imefikisha alama 70 baada ya mechi 26, wakiwa wamecheza mechi nne zaidi ya Simba SC waliopo nafasi ya pili kwa alama 57.

Wakati huo huo wakati Mzize akiwa kileleni katika mbio za ufugaji bora kupitia magoli 13, Prince Dube yupo nyuma yake kwa magoli 12.

Jean Charles Ahoua naye ana magoli 12,Jonathan Sowah magoli 11,Elvis Baranga Rupia magoli 10 na Steven Mkwala mabao tisa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news