MAPUTO-Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Msumbiji ambaye pia anaziwakilisha Madagascar na Ufalme wa Eswatini, Mheshimiwa CP Hamad Khamis Hamad leo Mei 27,2025 amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Morocco nchini Msumbiji,Mhe.Abdelali Rahali.
Wakati wa mkutano huo uliofanyika kwenye Ofisi za Ubalozi wa Morocco jijini Maputo, mbali ya Mhe. Balozi Hamad kujitambulisha kwa Mhe. Balozi Rahali,viongozi hao walikubaliana kushirikiana na kufanya kazi kwa ukaribu kwa maslahi ya Tanzania na Morocco.


