Balozi wa Jamhuri ya Muingano wa Tanzania nchini Msumbiji ambaye pia anaziwakilisha Jamhuri ya Madagascar na Ufalme wa Eswatini, Mheshimiwa CP Hamad Khamis Hamad amekutana na ndugu Akif Ali Khamis,Mkurugenzi Mkuu Shirika la Bandari Zanzibar (ZPC) na kujadiliana namna mamlaka zinazohusika na usimamizi wa bandari Msumbiji na Zanzibar zinavyoweza kushirikiana.