Balozi Kombo awasilisha ujumbe wa Rais Samia nchini Uganda

KAMPALA-Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo amewasilisha ujumbe Malumu kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwa Rais wa Jamhuri ya Uganda, Mheshimiwa Jenerali Yoweri Kaguta Museveni leo Mei 13,2025 mjini Entebbe,Uganda.
Waziri Kombo aliambatana na Balozi wa Tanzania nchini Uganda Mhe. Maj. Jen. Paul Kisesa Simuli.
Pamoja na mambo mengine, Waziri Kombo ametembelea majengo ya Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Kampala nchini Uganda yakijumuisha makazi ya awali ya Balozi yaliyopo Kololo.
Aidha, Waziri Kombo alihitimisha ziara yake kwa kufanya kikao kazi na Watumishi wa Ubalozi wakiongozwa na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Uganda, Mhe. Mej. Jen. Paul Kisesa Simuli, ambapo aliweka mkazo katika masuala muhimu ikiwa ni pamoja na utendaji na usimamizi mzuri wa rasilimali za Serikali, pamoja na kuibua fursa nyingi zilizopo kati ya Tanzania na Uganda.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news