MARA-Biashara United kutoka Musoma mkoani Mara imeshuka rasmi daraja kutoka Ligi ya Championship ya NBC mpaka First League.
Ni baada ya kucheza michezo 29 na kupata alama 15 ikifunga mabao 24 kufungwa mabao 43 na imebakiza mchezo mmoja ili kukamilisha msimu ambapo hata ikishinda haitaweza kupata alama za kuifanya kucheza play off.
Biashara United ilishuka daraja kutoka Ligi Kuu ya NBC katika msimu wa 2021/2022 ambapo ilitolewa na timu ya Azam baada ya kufungwa mabao 4-0 na kuwafanya kucheza Ligi ya Championship kwa misimu mitatu na sasa wameshuka kwenda Ligi ya First League.