DAR-Rais wa Heshima wa Simba SC na Mkurugenzi wa Bodi ya Simba SC,Mohamed Dewji (Mo Dewji) ameeleza kutoridhishwa na maamuzi yaliyotolewa na CAF ya kudai uwanja Benjamin Mkapa haufai kuchezewa fainali ya Kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya RS Berkane na badala yake mchezo huo utapigwa kwenye uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.
“Kwa mujibu wa vigezo vilivyotolewa, kila hatua ya ukarabati wa uwanja ilifuatwa kwa umakini ili kuhakikisha unakuwa tayari kwa mechi hiyo ya fainali.Wakati huo huo, baadhi ya matukio yaliyotokea nyuma ya pazia yameacha maswali ya msingi. Taarifa zilianza kusambaa mtandaoni kabla ya taarifa rasmi kutolewa. Tulieleza wasiwasi wetu kwa uwazi.
"Pamoja na juhudi hizi zote, CAF imethibitisha kuendeleza uamuzi wa kuhamishia fainali hiyo Zanzibar.
"Bila shaka, matokeo haya ni ya kusikitisha si kwa Simba tu, bali kwa mashabiki wetu, na kwa wote waliotoa juhudi kubwa kuandaa tukio hili katika historia ya Simba na Tanzania.Kwa mtazamo wangu wa kibinafsi, hatukutendewa haki.”

