Caroline Wanjiku Mwangi akamatwa na kilo 1.3 ya Cocaine uwanja wa ndege akielekea India

NAIROBI-Caroline Wanjiku Mwangi mwenye umri wa miaka 25 amekamatwa na maafisa wa Kupambana na Dawa za Kulevya katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi nchini Kenya kwa tuhuma za kusafirisha dawa za kulevya aina ya Cocaine.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo mwanamke huyo alikuwa akisafirisha kilo 1.3 za Cocaine kwenda nchini India.
Caroline alikamatwa wakati akijaribu kupanda ndege kwenda Goa. Goa ni jimbo lililopo Magharibi mwa India lenye mikondo ya pwani inayoenea kando ya Bahari ya Arabia.

Pia,jimbo hilo linasifika kwa matanuzi na shughuli za anasa zikijumuisha watu kutoka ndani nje ya nchi hiyo.
Aidha, imebainishwa dawa hizo zilipatikana kwenye mzigo wake ukiwa umefungwa.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari, Caroline yuko rumande katika Kituo cha Polisi cha JKIA, akisubiri kesi mahakamani, huku dawa hizo zikishikiliwa kama ushahidi.
Ikumbukwe kuwa, vita dhidi ya dawa za kulevya si kwa Taifa la Kenya tu, bali Tanzania kupitia Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) inaendesha operesheni kali angani, nchi kavu na baharini ili kuhakikisha hakuna anayesafirisha, kuingiza, kusambaza na kuuza dawa hizo ndani na nje ya nchi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news