Charles Hillary afariki dunia

DAR-Msemaji Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Charles Hillary, amefariki alfajiri ya leo Mei, 11 2025 katika Hospitali ya Muhimbili Mloganzila, alikokuwa akipatiwa matibabu.
Charles Hillary ni miongoni mwa watangazaji bora wa Redio na Televisheni nchini Tanzania ambaye amefanya kazi katika vituo mbalimbali vya ndani na nje ya Tanzania ikiwemo Radio One na ITV, BBC London na AzamTV.

Marehemu Charles Hilary alizaliwa Zanzibar miaka 66 iliyopita eneo la Jang’ombe. Mwaka 1968 alihamia jijini Dar es Salaam na kujiunga na Shule ya Msingi ya Ilala Mchikichini. Taarifa zaidi zitakujia punde.
Wakati huo huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan ametoa pole kutokana na kifo hicho.

"Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Bw. Charles Hilary, Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano Ikulu Zanzibar kilichotokea leo Mei 11, 2025.

"Ninatoa pole kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Hussein Mwinyi, familia, ndugu, jamaa na marafiki na wadau wote wa sekta ya habari nchini kwa msiba huu.
"Ndugu Charles Hilary atakumbukwa kwa mchango wake adhimu wa zaidi ya miaka 40 katika kukuza sekta ya habari nchini tangu akiwa redioni hadi kwenye televisheni, pamoja na unasihi kwa wanahabari wachanga.

"Namuomba Mwenyezi Mungu aijaalie familia yake uvumilivu na subra katika kipindi hiki kigumu, na ailaze roho ya mpendwa wetu mahala pema.

"Hakika sote ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake tutarejea."

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news