ARUSHA-Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) kwa kushirikiana na Asasi ya Bluecross Society of Tanzania imetoa mafunzo maalumu kwa wazazi 47 kutoka shule nane za jijini Arusha juu ya madhara ya tatizo la dawa za kulevya katika Ukumbi wa Kanisa la Anglikana jijini humo. 
Wazazi hao walielezewa mbinu za kumtambua mtoto ambaye ameshaanza kujihusisha na dawa za kulevya na jinsi ya kumuepusha na tatizo hilo.