RUKWA-Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), kupitia Ofisi ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, imetoa elimu kwa akinamama wajawazito na wanaonyonyesha katika Kituo cha Afya Mazwi, Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa.
Mafunzo hayo yalilenga kuwaelimisha juu ya madhara ya matumizi ya dawa za kulevya kwa mama na mtoto, hasa wakati wa ujauzito na baada ya kujifungua, sambamba na mbinu za kujenga familia salama isiyoathirika na matumizi ya dawa hizo.
Aidha, washiriki walifundishwa kuhusu malezi bora, mawasiliano kati ya mzazi na mtoto, pamoja na namna ya kuwalinda watoto dhidi ya bidhaa hatarishi zenye kemikali au dawa za kulevya kama biskuti, pipi, keki na vinywaji vinavyolenga watoto kwani baadhi ya bidhaa hizo huwalenga watoto kama soko la baadaye la dawa za kulevya, hali inayotishia ustawi wa taifa.
Tags
DCEA
DCEA Tanzania
Habari
Kataa Dawa za Kulevya na Timiza Ndoto Zako
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA)




