Mfalme Zumaridi akamatwa tena

MWANZA-Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limemkamata Diana Bundala (42) maarufu Mfalme Zumaridi, kwa tuhuma za kuendesha shughuli za kidini bila usajili rasmi na kusababisha usumbufu kwa wakazi wa Mtaa wa Buguku, Kata ya Buhongwa, Wilaya ya Nyamagana.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Wilbrod Mutafungwa ameeleza kuwa, Zumaridi amekamatwa Mei 15, 2025 majira ya saa nne asubuhi jijini Mwanza.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda Mtafungwa mbali na Zumaridi kutuhumiwa kuendesha shughuli za kidini bila kusajiliwa pia anahusishwa na video inayosambaa mitandaoni ikimuonesha akiwa na kundi la watoto wa kike na wa kiume huku akidai kuwa yeye ni Mungu wao na ana uwezo wa kuwalinda dhidi ya kifo.

"Uchunguzi unaendelea kwa kushirikiana na taasisi nyingine za serikali, tunawaomba wananchi wenye taarifa mbalimbali kusaidia uchunguzi watoe ushirikiano ili hatua stahiki za kisheria zitachukuliwa mara tu uchunguzi utakapokamilika."

Aidha, hii si mara ya kwanza Zumaridi kukamatwa na Jeshi la Polisi, kwani mwaka 2022 alituhumiwa kwa usafirishaji haramu wa binadamu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news