Dkt.Yonazi afika msibani kwa Hayati Msuya, atoa salamu za pole

DAR-Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi amefika msibani kwa Hayati Cleopa Msuya aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais na Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye aliyefariki tarehe 07 Mei, 2025 katika Hospitali ya Mzena jijini Dar es Salaam alipokuwa amelazwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa moyo.
Dkt. Yonazi amefika nyumbani kwa hayati Cleopa Msuya Upanga Jijijni Dar es Salaam akiongozana na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ally Senga Gugu na kutoa salamu za pole kwa familia ya Hayati Msuya.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news