UONGOZI, Menejimenti na watumishi wa Tume ya TEHAMA (ICTC) unaungana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dk. Samia Suluhu Hassan na Watanzania wote katika kuomboleza kifo cha Mhe. Cleopa David Msuya, Makamu wa Kwanza wa Rais na Waziri Mkuu Mstaafu.
