DOHA-Tanzania na Qatar zimekubaliana kuimarisha ushirikiano katika masuala ya ajira baada ya kikao kati ya Balozi wa Tanzania nchini Qatar, Habibu Awesi Mohamed, na Naibu Katibu wa Wizara ya Kazi wa Qatar, Sheikha Najwa bint Abdulrahman Al Thani.

Katika kikao kilichofanyika Doha, Balozi Awesi alitoa pongezi kwa Serikali ya Qatar kwa nafasi za ajira inazotoa kwa Watanzania, akitangaza kuwa madereva 800 wa Kitanzania watafanyiwa usaili na kampuni ya Mowasalat Karwa kuanzia Mei 22 hadi 25, 2025 jijini Dar es Salaam. Pia aliomba msaada wa kurahisisha utoaji wa Visa kwa watakaochaguliwa.


















Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo