Aliyekuwa Mbunge wa Mlimba, Suzan Kiwanga, viongozi wengine watatu na wanachama 50 wa Wilaya za Kilosa na Kilombero na wanachama 50 mkoani Morogoro wametangaza kuondoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Mbali na Suzan ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake la Chadema (BAWACHA), wengine ni Mwenyekiti wa BAWACHA Wilaya ya Kilombero, Magreth Lipindi, Mwenyekiti wa BAVICHA Wilaya ya Kilosa, David Chiduo, ambaye pia aliwahi kuwa Diwani wa Kata ya Viwanja Sitini na aliyekuwa Mwenyekiti wa BAWACHA Wilaya ya Kilosa, Sheila Mkubwa.
Viongozi hao wametangaza uamuzi huo Mei 13,2025, wakieleza sababu kubwa ni msimamo wa CHADEMA kutoshiriki Uchaguzi Mkuu Oktoba mwaka huu, wakiendelea kushikilia msimamo wa No Reforms No Election.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo




















