NAIROBI-Serikali ya Kaunti ya Nairobi nchini Kenya imefunga jengo la Freemasons Hall la Grand Lodge of East Africa lililoko katikati ya jiji kutokana na deni la kodi ya ardhi lililofikia Ksh. milioni 19 (shilingi milioni 396.6 za Kitanzania).
Operesheni hiyo imeongozwa na Mjumbe wa Kamati ya Afya katika Baraza la Mawaziri wa Kaunti, Suzanne Silantoi, ikiwa ni sehemu ya kampeni ya kaunti dhidi ya wadaiwa wa kodi, aliyeongozana na maafisa wengine ambao walisema taratibu zote zilifuatwa kabla ya kufunga jengo hilo ikiwa ni pamoja na kutuma barua na kutoa ilani za madai na matangazo kwenye magazeti.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo























