DAR-Wajumbe wa Sekretarieti ya CHADEMA iliyomaliza muda wake akiwemo aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Bara, Benson Kigaila, aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu CHADEMA Zanzibar, Salum Mwalimu, Catherine Ruge na aliyekuwa Mkurugenzi wa Itifaki na Mawasiliano, John Mrema ambao walitangaza kujiondoa CHADEMA kuanzia Mei 7,2025 hatimaye wamehamia rasmi Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) wakiwa pamoja na wengine akiwemo Devotha Minja.
Mwenyekiti wa CHAUMMA,Hashim Rungwe amewapokea wanachama hao wapya na kuwakabidhi kadi za CHAUMMA jijini Dar es Salaam Mei 19,2025 kwenye Mkutano Mkuu wa CHAUMMA.

Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo