Rais Dkt.Samia ateua viongozi mbalimbali

DAR-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali akiwemo Prof. Tumaini Nagu ambaye ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia masuala ya afya.
Aidha,Dkt.Blandina Kilama ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango anayeshughulikia biashara na ubunifu.

Dkt.Kilama anachukua nafasi ya Dk. Lorah Madete ambaye uteuzi wake umetenguliwa na atapangiwa majukumu mengine.

Balozi George Madafa ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Puma Energy Tanzania akichukua nafasi ya Dkt.Majige Budeba ambaye amemaliza muda wake.

Jacob Kibona ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) kwa kipindi cha pili.

Kwa upande wake Meja Jenerali Mstaafu John Mbungo akiteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Meli Tanzania (TASHICO) kwa kipindi cha pili.

Vilevile,Mussa Mandia ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) kwa kipindi cha pili.

Aidha,uapisho wa Naibu Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mtendaji utafanyika kwa tarehe itakayopangwa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news