DAR-Msanii maarufu wa filamu nchini na Mkurugenzi wa Taasisi ya Wema wa Mama, Wema Sepetu, ameomba radhi kwa kuvaa mavazi yaliyozua mjadala kuhusu maadili na kuahidi kuwa tukio hilo halitarudiwa tena.
Wema ameyasema hayo baada ya kuitikia wito wa Bodi ya Filamu Tanzania kufuatia picha zake zilizosambaa mitandaoni na kuzua mijadala mikali kuhusu maadili ya wasanii.

Akizungumza baada ya kikao hicho, Wema alisema kilikuwa si kikao rasmi cha kisheria bali ni cha mazungumzo ya kukumbushana kuhusu maadili ya wasanii nchini.
“Nilikuja Bodi ya Filamu kuitikia wito. Kikao hakikuwa rasmi, bali kilikuwa cha kukumbushana juu ya maadili. Nimeyasikia na nimeyazingatia.
“Kufanya kosa si kosa, bali kurudia kosa ndio kosa. Nachukua nafasi hii kuomba msamaha kwa wote niliowakwaza. Nimejifunza, na haitajirudia tena,” alisisitiza Wema.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo