DAR-Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda, amezindua mradi wa awamu ya pili wa ujenzi na uendelezaji wa Kituo cha Umahiri wa Sayansi ya Magonjwa ya Moyo na Mishipa ya Damu kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki, unaotekelezwa na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS).

Mradi huo unatekelezwa katika Kampasi ya Mloganzila ya MUHAS, ukigharimu dola milioni 83 kupitia mkopo kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), na unasimamiwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia. kupitia mradi huu, hospitali ya kisasa ya magonjwa ya moyo na mishipa ya damu itajengwa pamoja na kuwekwa vifaa tiba vya kisasa.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo















