DODOMA-Waziri wa Elimu,Mheshimiwa Prof. Adolf Mkenda leo Mei 12,2025 amewasili bungeni jijini Dodoma kwa ajili ya kuwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa mwaka wa Fedha 2025/2026.
Bajeti hii inatarajiwa kuwa ya kihistoria kutokana na mageuzi makubwa yanayoendelea katika sekta ya elimu nchini.


