Prof.Janabi ashinda kwa kishindo WHO Afrika, who is Prof Janabi?

NA DIRAMAKINI 

MSHAURI wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika masuala ya Afya na Tiba, ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili,Profesa Mohamed Janabi ameshinda uchaguzi wa nafasi ya Ukurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Kanda ya Afrika.
Ni katika kikao maalum cha pili kilichoketi leo Mei 18, 2025 jijini Geneva nchini Uswisi. Profesa Janabi ameshinda kwa kura 32 kati ya kura 46 ambapo alikuwa akichuana na N’da Konan Michel kutoka Ivory Coast.

Mohammed Lamine kutoka Guinea, Dkt. Boureima Hama Sambo kutoka Niger, Profesa Moustafa Mijiyawa kutoka Jamhuri ya Togo.

Profesa Janabi ameshinda nafasi hiyo iliyoiachwa wazi na aliyekuwa Mkurugenzi Mteule, Dkt.Faustine Ndugulile ambaye alifariki Novemba 27, 2024.

Aidha, Profesa Janabi anakuwa Mtanzania wa pili kushika nafasi hiyo ya juu kwenye shirika hilo kwa Ukanda wa Afrika.

Profesa Janabi ambaye ni daktari wa magonjwa ya moyo na msimamizi wa afya anayeheshimika zaidi Tanzania amekuwa na jukumu muhimu katika kuunda hali ya matibabu nchini.

Pia,uzoefu wake ni wa miongo kadhaa ikiwa ni pamoja na kuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete na baadaye Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili umeleta matokeo chanya katika sekta ya afya nchini.

Katika hatua nyingine,Wizara ya Afya imetuma pongezi kwa Profesa Janabi na kumsifia kama mgombea aliyestahili kushinda nafasi hiyo.

‘‘Tunafurahia kuchaguliwa kwa Prof. Mohamed Janabi kuwa Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika. Shukrani kwa Afrika kwa uungwaji mkono wa kiwango cha juu."

Who is Prof Mohamed Yakub Janabi?

Prof Mohamed Yakub Janabi of Tanzania has been elected as the new Regional Director for Africa at the World Health Organization (WHO), following a vote by the WHO Regional Committee for Africa in Geneva. Here is Prof Mohamed Yakub Janabi Curriculum Vitae (CV);

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news