ZANZIBAR-Rais wa Msumbiji Mheshimiwa Daniel Chapo tayari amewasili Zanzibar akitokea jijini Dar Es Salaam ambapo akiwa Zanzibar atakua na ziara fupi ya kikazi.

Rais Chapo atakutana na Mwenyeji wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi pamoja na kutembelea kituo cha Uvuvi cha Bahari kuu Fumba.