ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amewasili Zanzibar akitokea Zimbabwe, ambako alishiriki Kikao cha Wakuu wa Nchi na Viongozi wa Serikali wa Nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) kilichojadili Uhifadhi wa Hifadhi zinazovuka mipaka.
Alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Leo tarehe 24 Mei 2025 alipokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Idrisa Kitwana Mustafa, pamoja na baadhi ya viongozi wa Serikali na Wakuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama.




