DAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amejumuika na Viongozi Wakuu wa Serikali katika Dhifa ya Chakula cha Usiku iliyoandaliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa heshima ya Rais wa Namibia, Mhe. Dkt. Netumbo Nandi-Ndaitwah.
Hafla hiyo imefanyika Ikulu, jijini Dar es Salaam tarehe 20 Mei 2025.




