Rais Dkt.Samia afanya uteuzi na uhamisho wa viongozi mbalimbali

DAR-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uhamisho na uteuzi wa viongozi mbalimbali. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, uhamisho na uteuzi huo ni kama ifuatavyo:
Rais amemhamisha kituo cha Kazi Mhe. Albert Gasper Msando kutoka Wilaya ya Handeni kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo mkoani Dar es Salaam.

Mhe. Japhari Mghamba Kubecha amehamishwa kutoka Wilaya ya Tanga kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Handeni mkoani Tanga.

Aidha, Rais amemhamisha Mhe. Dadi Horace Kolimba kutoka Wilaya ya Karatu kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Tanga;

Rais Samia amemteua Ndg. Lameck Karanga Nganga kuwa Mkuu wa Wilaya ya Karatu. Kabla ya uteuzi huu, Bw. Nganga alikuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Karatu.

Naye Ndg. Bahati Migiri Mfungo ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Karatu. Kabla ya uteuzi huu, Bw. Mfungo alikuwa Afisa Tarafa ya Mbuguni, Wilayani Arumeru.

Pia amemteua Ndg. Lazaro Jacob Twange kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO). Kabla ya uteuzi huu, Bw. Twange alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo.

Katika uteuzi mwingine, Rais amemteua Ndg. Andrew William Massawe kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA). Bw. Massawe anachukua nafasi ya Jaji Mkuu Mstaafu Mhe. Mohamed Chande Othman ambaye amemaliza muda wake.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news