Rais Dkt.Samia kuzindua Sera mpya ya Mambo ya Nje kesho

NA GODFREY NNKO 

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuzindua Sera mpya ya Mambo ya Nje ikiwa ni zao la maboresho ya Sera ya mwaka 2001 (Toleo la 2024 la Sera ya Mambo ya Nje ya Mwaka 200).

Rais Dkt.Samia atashiriki katika tukio hilo muhimu ambalo litaangazia mwelekeo mpya wa Diplomasia ya Tanzania katika karne ya 21.
Hafla ya uzinduzi huo itafanyika kesho Mei 19,2025 katika Ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.

Mei 7,2025 jijini Dar es Salaam Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo aliwaeleza wahariri wa vyombo vya habari kuwa,litakuwa ni tukio muhimu hususani wakati huu Tanzania inapiga hatua kubwa katika sera yake ya mambo ya nje.

Balozi Kombo alisema,Sera ya Mambo ya Nje ya mwaka 2001 imefanyiwa marekebisho ili kuendana na mabadiliko mbalimbali duniani ambapo pia, wadau mbalimbali walishiriki kutoa maoni na mapendekezo.

Sera mpya imejumuisha mambo kadhaa ikiwemo kulinda maslahi ya taifa kisiasa, kiuchumi na kijamii kwa kuzingatia misingi ya uhuru,haki za binadamu, demokrasia na ujirani mwema.

Vilevile, inalenga kukuza diplomasia ya uchumi, kulinda maslahi ya taifa, kuendeleza uhusiano na nchi na taasisi mbalimbali na kuchangia maendeleo duniani.

Balozi Kombo pia alibainisha kuwa,sera mpya imelenga kujenga mazingira wezeshi ya ndani, kuimarisha ushirikiano wa kimataifa.

Pia kushughulikia masuala ya madeni, kuimarisha ushirikiano wa kikanda na kimataifa na kudumisha misingi ya sera ya kutofungamana na upande wowote duniani.

Diplomasia

Uzinduzi huu unakuja katika kipindi ambacho, Mheshimiwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan anaendelea kusalia kuwa shujaa zaidi kwa kuimarisha Diplomasia ya Tanzania kote Duniani.

Ikumbukwe, tangu Mheshimiwa Rais Dkt.Samia aingie madarakani mwaka 2021 amefanikiwa kurejesha uhusiano wa kimataifa, kuvutia uwekezaji, na kuimarisha ushirikiano wa kikanda na kimataifa.

Jitihada hizo zimesaidia kuboresha uchumi, kuongeza nafasi ya Tanzania kimataifa na kukuza amani na usalama ndani na nje ya nchi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news