DAR-Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Mei 17, 2025 amekagua ukarabati wa uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam ikiwa ni muendelezo wa ziara zake za kukagua maboresho ya viwanja kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya AFCON na CHAN yanayotarajiwa kufanyika nchini hivi karibuni.
Waziri Mkuu amesema kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na wakandarasi wanaokarabati uwanja huo ni kuwa upo tayari kwa michezo yoyote hata ya kimataifa na kwamba utakamilika kabla ya kuanza kwa mashindano ya CHAN na AFCON.
Kwa upande wa Tanzania Bara alikagua viwanja vya Shule ya Sheria, Gymkhan na Jenerali Isamuhyo.
Alisema uamuzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi wa kuridhia michuano hiyo kufanyika nchini utasaidia kwa kiasi kikubwa kuendeleza na kukuza sekta ya michezo na utalii nchini.