Rashid Mijuza ateuliwa kuwa Kaimu Meneja wa Uwanja wa Benjamin Mkapa

DAR-Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi amemtangaza rasmi Bw. Rashid Mijuza kuwa Kaimu Meneja wa Uwanja wa Benjamin Mkapa baada ya kumhamisha na kumpeleka Makao Makuu ya Wizara hiyo aliyekuwa Meneja wa Uwanja huo Bw. Malinde Mahona ambaye atakuwa msimamizi wa viwanja vyote nchini.
Waziri Kabudi amesema hayo Mei 10, 2025 alipofanya ziara maalumu ya ukaguzi wa Kiwanja hicho na viwanja vya Mazoezi ya CHAN 2024 akiongozana na Katibu Mkuu Wizara hiyo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa jijini Dar es salaam.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news