Serikali kufikisha maji katika makazi Msomera

TANGA-Serikali imejipanga kuhakikisha huduma ya maji inaimarishwa kwa wananchi walioamua kuhamia eneo la Msomera, Handeni.Naibu Katibu Mkuu Bi. Agness Meena akiongea kwa Niaba ya Waziri wa Maji kuhusu huduma ya maji amesema kazi kubwa inafanyika kuhakikisha miundombinu ya maji inafika katika maeneo yote ya makazi pamoja na kujenga mabirika ya mifugo.
Amesema kazi ya ujenzi inafanyika kwa awamu na hivi sasa ni awamu ya nne, ambapo bwawa la maji la Msomera pamoja na kutoa huduma lipo katika hatua za mwisho za utekelezwaji pamoja na matanki ya ukubwa mbalimbali ya kuhifadhi maji.

Msimamizi wa mradi wa RUWASA Mhandisi Nobert Temba ameainisha usanifu wa kazi hiyo ni uwezo wa kuhudumia bila tatizo kwa miaka 20.
Bi. Meena katika ukaguzi wa kazi hiyo ameongozana menejimenti ya Wizara ya Maji, RUWASA na uongozi wa wananchi wa Msomera.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news