ZANZIBAR-Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaana Idara Maalum za SMZ Mhe. Masoud Ali Mohamed amesema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imepanga kukiimarisha kituo cha KMKM Sengenya kiswani Pemba kupitia Mradi wa Ujenzi wa Mahanga na Ofisi za KMKM.
Akijibu swali la Mhe. Dkt. Mohammed Ali Suleiman (Muwakilishi Jimbo la Mtambwe) huhusu kukiboreha kituo cha KMKM Sengenya katika Baraza la Wawakilishi Chukwani 08/05/2025 amesema, mchakato wa kuimarisha kituo hicho utaanza rasmi katika Bajeti ya mwaka wa fedha 2025/2026, hatua ambayo itajumuisha upatikanaji wa vitendeakazi vya kisasa.
Aidha,Mheshimiwa Maoud ameeleza kua Kituo cha KMKM Sengenya ni miongoni mwa vituo vya ulinzi vya Kikosi Maalumcha Kuzuia Magendo(KMKM) ambacho kinaendelea kutoa huduma kwa uweledi na ufanisi kwa kufanya shughuli za ulinzi na udhibiti wa magendo.
Amesema, hali ya Kituo cha KMKM Sengenya haikwamishi operesheni za Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo (KMKM) kwa vile kituo hicho ni sehemu ya vituo vyengine mbali mbali vya KMKM vilivyopo nchini.
Hivyo, kituo hicho kinaendelea na kazi zake za kawaida na opereshesni maalum kadri itakavyohitajika kama ilivyovituo vyengine vya KMKM.
