Viwanja vyote vipo tayari kwa CHAN-Naibu Waziri Mwinjuma

DODOMA-Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamis Mwinjuma, amesema kuwa maandalizi ya Kombe la Mataifa Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) yanaendelea kwa kasi, huku viwanja vyote vilivyopangwa kwa ajili ya mashindano hayo vikiwa tayari kwa matumizi hata kama michuano ingeanza mwezi ujao.
Kauli hiyo ametoa leo Mei 30, 2025 Bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Makete, Festo Sanga, aliyeomba kuhakikishiwa kama Tanzania ipo tayari kwa CHAN inayotarajiwa kufanyika Agosti 2025.

Viwanja hivyo ambavyo Mheshimiwa Mwinjuma amesema vimekamilika ukarabati wake ni Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam, Amaan Zanzibar na viwanja vya mazoezi ambapo Dar es salaam kuna viwanja vitatu kikiwemo Shule ya Sheria, Gymkana na Meja Jenerali Isamuhyo ambavyo vyote vipo katika hali nzuri.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news