Wajionea utekelezaji wa shughuli za kilimo hifadhi

DODOMA-Wizara ya Kilimo kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo ya kilimo hifadhi nchini, wakiwemo Diocese of Central Tanganyika (DCT), Community Facilitation Unit (CFU), World Renew, Nachingwea Development Organisation (NADO) na Tanzania Agricultural Research Institute (TARI), imefanya ziara hivi karibuni katika Kata ya Hombolo, jijini Dodoma, kwa lengo la kujionea utekelezaji wa shughuli za kilimo hifadhi.
Katika ziara hiyo, washiriki walitembelea vikundi vya akiba na mikopo vinavyowawezesha wakulima wadogo kuongeza kipato na kuboresha uzalishaji. Vikundi hivyo vinatekelezwa chini ya Diocese of Central Tanganyika (DCT) kwa ufadhili wa CFGB Tearfund kutoka Canada.

Kupitia ufadhili huo, wakulima wamepatiwa zana za kisasa za kilimo hifadhi kama vile “power tillers” pamoja na mafunzo ya mbinu bora za kilimo, ikiwa ni sehemu ya kuimarisha tija na ustahimilivu wa sekta ya kilimo.

Kata ya Hombolo inajivunia uzalishaji wa mazao jamii ya mikunde, yakiwemo choroko, fiwi, mbaazi na kunde, ambayo yameendelea kuwa chanzo kikuu cha chakula na kipato kwa wakulima wa eneo hilo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news