BERLIN-Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Ujerumani, Mhe. Hassani Mwamweta amempokea ubalozini Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb) aliyefika nchini humo kwa ziara ya kikazi.
Mhe. Tax yuko Berlin, Ujerumani kushiriki Mkutano wa Mawaziri wa Ulinzi wa Nchi zinazoshiriki Operesheni za Amani za Umoja wa Mataifa (UN Peacekeeping Ministerial Conference 2025) kuanzia tarehe 13 hadi 14 Mei, 2025.Katika mazungumzo yao, Mhe. Mwamweta na Mhe. Tax wamejadili masuala mbalimbali yahusuyo uhusiano wa Tanzania na Ujerumani pamoja na ushiriki wa Tanzania katika operesheni za kulinda amani duniani.



