Wizara kutoa elimu kwa jamii kuhusu ardhi na makazi

ZANZIBAR-Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi imesema imejipanga kutoa elimu kwa jamii kuhusu masuala ya Ardhi na Makaazi kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii ili kupunguza migogoro inayotokana na kadhia hiyo.
Akisoma Makadirio ya Mapatona matumizi kwa mwaka wa fedha 2025/2026 Waziri wa Wizara hiyo Mhe Rahma Kassim Ali amesema kuwa migogoro ya ardhi kwa jamii imekuwa ikijitokeza mara kwa mara hivyo elimu hiyo itasaidia kupunguza tatizo hilo.

Amesema kuwa Serikali imejipanga kuendelea na utambuzi wa ardhi pamoja na uandaaji wa mipango mikuu na ya kina kwa matumizi ya ardhi ya miji mbalimbali Unguja na Pemba.

Aidha amesesema kuwa wataendelea na zoezi la kliniki ya Ardhi kwa shehia mbalimbali Unguja na Pemba ili kuwafikia wananchi wa chini kwa kuwajengea uelewa juu ya utoaji wa huduma za ardhi, utatuzi wa migogoro ya Ardhi pamoja na masuala mengineyo yanahusiana na sekta ya ardhi nchini.

Waziri Rahma ameeleza kuwa wataendelea na ujenzi wa mifumo ya utoaji wa huduma kwa wananchi katika Sekta ya Ardhi na Makaazi pamoja na ujenzi wa nyumba mpya za Makaazi na biashara pamoja na kufanya matengenezo ya nyumba zilizopo.

Hata hivyo amefahamisha kuwa hadi kufikia Machi 2025 program ndogo imefanikiwa kutekeleza kazi mbalimali kwa kuratibu na kusimamia utekelezaji wa miradi ya wizara ikiwemo mradi wa usimamizi na usajili wa taarifa za ardhi (LARIS)pamoja na ujenzi wa nyumba za makazi ikiwemo nyumba za Chumbuni,na Kiembesamaki.

Aidha ameeeleza kuwa Wizara imeratibu uandaaji wa sera ya miji na maendeleo ya makazi ambapo rasimu ya sera hiyo imekamilika na ipo katika hatua ya kuwasilishwa katika vikao vikao vya maamuzi.

Waziri Rahma amesema wanaendelea kufuatilia utekelezaji wa miradi ya Wizara na Taasisi zake ikiwemo mradi wa nyumba za makazi 72Mombasa9kwa Mchina),mradi wa jengo la makazi na biashara Darajani, mradi wa matengenezo ya nyumba namba 1699/1705 mnadani awamu ya kwanza na mradi wa Mkungu Malofa Chakechake Pemba.

Akitoa hotuba ya maoni ya Kamati Mwenyekiti wa Kamatiya Mawasiliano, Ardhi na Nishati Baraza la Wawakilishi Mhe, Yahya Rahid Abdulla ameiomba Wizara kuongeza jitihada za kusikiliza na kutoa maamuzi juu ya mashauri yote yanayohusiana na migogoro ya ardhi iliyopo Mahakamani na mengine ambayo ipo katika jamii kwa kuzingatia misingi ya haki, weledi na uadilifu bila ya kudhulumu upande wowote.

Waziri Rahma ameliomba Baraza limuidhinishie jumla ya sh bilioni 345,485,900,000 ili kutekeleza kazi za kawaida na kazi za maendeleo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news