DODOMA-Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi leo Mei 19,2025 imehamia rasmi katika jengo lake jipya lililopo katika mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Deogratius Ndejembi pamoja na Katibu Mkuu wa wizara hiyo Mhandisi Anthony Sanga waliwaongoza watumishi wa wizara hiyo kuhamia kwenye jengo hilo."Leo hii sisi tumehamia rasmi na tuko tayari kwa ajili ya kutoa huduma kwa wananchi na wote wanaokuja katika ofisi zetu basi wakaribie hapa Mtumba kwa sababu sasa majukumu rasmi yatakuwa yakitolewa hapa," amesema Mhe. Ndejembi.






