Wizara ya Elimu yaomba kuidhinishiwa shilingi trilioni 2.4 kwenda kukoleza kasi ya mageuzi Sekta ya Elimu nchini

DODOMA-Ili kuwezesha utekelezaji wa malengo yaliyoanishwa kwa mwaka wa fedha 2025/26, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Taasisi zake imeomba Bunge kuidhinisha makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa fedha 2025/2026 yenye jumla ya shilingi Trilioni 2.439.
Kati ya fedha hizo shilingi Bilioni 688.6 ni kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida ya Wizara ambapo Shilingi Bilioni 635.2 ni kwa ajili ya Mishahara na Shilingi Bilioni 53.3 ni kwa ajili ya Matumizi Mengineyo.
Hayo yamebainishwa leo Mei 12,2025 na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof Adolf Mkenda (Mb) wakati akiwasilisha bungeni jijini Dodoma Makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo.

Amesema kati ya fedha zinazoombwa, zaidi ya shilingi Trilioni 1.7 zinaombwa kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo ambapo Shilingi 1.186 ni fedha za ndani na Shilingi 560.8 ni fedha kutoka kwa Washirika wa Maendeleo.
Waziri Mkenda amesema kuwa Wizara kupitia Tume ya Taifa ya UNESCO imeomba kuidhinishiwa jumla ya Shilingi Bilioni 3.2 kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida ambapo Mishahara ni Shilingi Bilioni 1.5 na Matumizi Mengineyo ni Shilingi Bilioni 1.7164.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news